Kiswahili kimepandishwa cheo kuwa lugha ya Kimataifa

Lugha ya Kiswahili ilipandishwa hadhi na umoja wa mataifa (UN) na sasa ni lugha ya kimataifa na hivyo Kila tarehe saba Julai itakuwa inasherehekewa na ulimwengu mzima.

Ni ukweli kuwa lugha hii inazidi kuwa kwa kasi zaidi na sasa Kiswahili ni sawia na Kiingeereza ,Kijerumani ,Kifaransa Miongoni mwa lugha zingine.

Kwa upande mwingine lugha hii inakumbwa na matatizo chungu nzima.Mwanzo ni athari ya lugha ya sheng hasa kwa vijana mitaani.Vilevile sera za kuilinda lugha hii hazitiliwi maanani.

Kutokana na haya wakereketwa na maashiki wa lugha hii ashirafu ya Kiswahili wanaombwa kutiliwa maanani lugha hii ya Kimataifa.Vilevile ,wanazidi kutoa madai kwa kila mmoja kujiunga na vyama vya Kiswahili ili kuzidi kupigania lugha hii ya Kimataifa.

Leave a Reply and Don't Forget to Save your Logins.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.